Monday, October 10, 2016

Uchunguzi wa kifo cha mchezaji aliefariki baada ya kupigwa na mpira shingoni kuanza rasmi Australia.

Uchunguzi rasmi juu ya kifo cha mcheza Kriketi Philip Hughes unatarajiwa kuanza rasmi nchini Australia.


Mchezaji huyo alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kupigwa na mpira shingoni wakati wa mchezo huoJijini Sydney ambapo jeraha alilopata lilisababisha ubongo wake  kuchanganyika na damu na kumsabishia kifo siku mbili baadae.


Wachunguzi watachunguza kama kulikua na uwezekano wa kutumia kifaa kingine cha kuuokoa maisha ya mchezaji huo kwani mapema mwaka huu tathmini huru ilionesha kuwa kutumia kofia ngumu na ya kisasa ingeweza kuzuia ajali hiyo iliyopelekea kifo cha mchezaji huyo.
-BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.