Sunday, October 9, 2016

PICHA:Unaweza kuinunua Bibilia iliyokua ikitumiwa na Tupac gerezani kwa kiasi cha $54,000.

Bibilia iliyokuwa ikitumiwa na rapper Tupac alipokua Jela kutokana na makosa ya unyanyasaji wa kingono mwaka 1995 ipo sokoni na inauzwa mtandaoni kwa kiasi cha $54,000.


Dalali mmoja nchiini Marekani kupitia online site yake inayofahamika kama Moments In Time ameweka picha ya Bibilia hiyo ambayo Hayati  Tupac ameweka saini yake kwa maandishi ya kalamu nyekundu pamoja namba yake kama mfugwa #95A1140.

Katika mtandao huo picha za Bibilia hiyo zimeambatana na maelezo yanayosomeka,"The bible Tupac used while incarcerated in Dannemora for rape,signed on the front cover with his inmate  beneath his signature".



Tupac alihukumiwa kwenda Jela kwenye gereza lililofahamika kama Clinton Correctional Facility mnamo Feb. 15,1995 ambapo muda mfupi baada ya kuhukumiwa aliachia album yake inayofahamika kama "Me Against The World" ambayo wiki moja baada ya kutoka kwa album hiyo ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard 200.


Hii sio mara ya kwanza kwa vifaa au vitu vinavyohusiana na rapper huyo mkongwe anaetajwa kuufanya muziki wa Hip Hop kujulikana ulimwenguni kuuzwa mtandaoni,Kwani baadhi barua na nyimbo zilizoandikwa kwa mkono wake zimewahi kupigwa mnada mtandaoni.

Tupac alifariki mwaka 1999 baada ya kupigwa risasi alipokua akitoka kutazama pambano la ngumi la swahiba wake,Mike Tyson.


“The Bible Tupac used while incarcerated in Dannemora for rape, signed on the inside front cover with his inmate # beneath his signature.”

Read More: Tupac Shakur’s Prison Bible Being Sold for $54,000 - XXL | http://www.xxlmag.com/news/2016/10/tupac-shakurs-bible-being-sold/?trackback=tsmclip

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.