Katika hali ambayo ni ya kushangaza Walimu wa Shule ya Sekondari Lugalo
iliyopo Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo
cha Polisi Jamii wameunasa mtandao wa Wanafunzi wa kike na wa kiume
wanaojihusisha na uvutaji wa madawa ya kulevya hasa bangi na kunjwa
pombe kali aina ya "Viroba" wakati na baada ya vipindi vya darasani.
Msako huo umekuja baada ya Walimu wa Shule hiyo
kuwahisi kuwa huenda wanafunzi wao wanavuta bangi,kutokana na mabadiliko ya kitabia waliyaonesha Shuleni hapo.
Inadaiwa kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo baada ya kutoridhika na majibu ya wanafunzi,akaamua
kuandaa kikosi cha walimu kwa kushirikiana na Polisi Jamii kufanya
uchunguzi kuhusu suala hilo ambapo baadhi ya wananchi wenye nia njema walitoa taarifa Shuleni hapo kuwa
kuna wanafunzi ambao huwa wanawaona wakivuta bangi kwenye milima
iliyopo pembeni kidogo na shule na Shule hiyo.