Mwanamuziki Vanessa Mdee amewaongoza mabinti wa Kitanzania kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani nchini wakishiriki mdahalo uliandaliwa na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ukiwajumuisha wasichana kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambapo mada kuu katika mdahalo huo mwaka huu ni 'Umuhimu wa Elimu Kwa Msichana'