Monday, October 31, 2016
Zimbabwe kutumia sarafu ya China 'Yeun' ili kulipa deni la $40m.
Waziri wa fedha wa nchi hiyo alitangaza uamuzi huo baada ya Gavana wa Benki kuu ya Zimbabwe John Mangudya kudai kuwa mpango huo utupunguza mzigo wa madeni ya nchi hiyo kwa wahisani wake wa kiuchumi.
Hata hivyo wananchi wengi bado hawajaridhishwa na uamuzi huo wa kutumia sarafu ya China 'Yuan' kwenye matumizi yao ya kila siku,mpango unaotarajiwa kuanza mwezi januari mwakani,Ambapo China taifa linalotajwa kuwa na uchumi imara kutoka bara la Asia limedai litapunguza deni la $40m.
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo wamepinga uamuzi huo na kudai kuwa serikali ya chama cha ZANU (PF) inayoongozwa na Rais Robert Mugabe imeishiwa sera ya kuliongoza taifa hilo.
Comments System
facebook