Wachina walizwa Sh22.8 milioni na tapeli aliejitambulisha kama Paul Makonda.
Raia wa China wametapeliwa fedha
taslimu Sh22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya
kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba
Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye ni raia wa
China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni
Makonda.
Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia
huyo atoe Dola 3,500 za Marekani kwa ajili ya msaada wa kumsomesha
mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manilla kilichopo
nchini Ufilipino.
“Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jensen
Hung (39) alikubali ombi la mkuu wa mkoa huyo feki na kumtuma msaidizi
wake, Marco Li aende ofisini kwake kwa ajili ya kujiridhisha,” alisema Kamanda
Sirro.