Tuesday, November 1, 2016

Serikali kuja na mpango huu unaowahusu Wanaume wanaoshiriki mapenzi ya Jinsia moja.





DAR ES SALAAM - Tanzania,Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wanawake,Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema mpango huo uliondaliwa na serikali na maalumu kwa ajili ya kuwaelemisha wanaume  wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ili kuepukana na athari zinazotokana na vitendo hivyo hasa maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mwandishi wa mtandao wa Reuters,Waziri Ummy amedai kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kuwepo taarifa za kuwepo kwa baadhi ya mashirika ya misaada (NGOs) ambayo yamekua yakiendesha kampeni zinazohamasisha mapenzi ya jinsia moja na kudai kuwa vitendo vya 'Ushoga' ni kinyume na sheria za nchi ambapo mtuhumiwa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela.



Hata hivyo ameongeza kuwa Serikali itaendelea na kampeni yake ya kupambana na Ugojwa wa UKIMWI kwa vijana na makundi mengine ndani ya jamii.

Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya,Tanzania ina jumla ya Watu milioni 1.4 wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI,idadi ambayo ni sawa na % 5 ya raia wote,huku maambukizi yanayosababishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja yakipanda kwa %25.





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.