Kanisa la kihistoria la 'Greenville',Missisippi lilivamiwa na watu zaidi ya 200 majira ya saa tisa usiku mnamo tarehe 1,Mwezi Novemba,2016 ambapo wavamizi hao walichoma moto sehemu ya jengo ya Kanisa hilo na kuacha ujumbe wa maandishi kwenye ukuta iliosomeka 'VOTE FOR TRUMP'.
Mpaka sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kwa tukio hilo,ils mashuhuda wamekua wakihojiwa na Maafisa wa Usalama wa FBI.
Hata hivyo shambulizi linatafriwa kama muendelezo wa shambulizi jingine lililofanyika kwenye makao makuu ya Chama Republican ambacho Bwn. Trump anakiwakilisha kwenye uchaguzi,huko North Carolina.
Kingine kizuri ni kwamba mara baada ya kutokea kwa tukio hilo Watu wema wameanzisha kampeni inayofahamika kama 'GoFundMe' kwa ajili matengenezo ya Kanisa hilo kongwe,kampeni iliyopangwa kukusanya kiasi cha $10,000,ila cha ajabu siku ya kwanza kampeni hiyo ilikusanya zaidi ya $169,000.
....!!..Kisasi hakizidi Wema.