Baada ya Mgombea wa Chama cha Republican,Donald Trump kuandamwa na Kashfa ya kuwadhalilisha Wanawake kingono sasa ubao umemgeukia Mgombea wa Chama cha Domacratrict,Bi.Hillary Clinton ambae barua pepe zinazodaiwa aliziandika ili kuchangisha michango ya ufadhili wa Kundi la kigaidi la ISIS zimevuja.
Kwa mujibu wa tovuti ya.http://www.redflagnews.com/headlines-Barua pepe hizo,zimevujishwa na mtandao wa 'WeakLeak' uliofungiwa nchini Marekani ambapo Mwanzilishi wa mtandao huo Julian Assange yupo uhamishoni kama mkimbizi nchini Urusi.
“The governments of Qatar and Saudi Arabia, which are providing clandestine financial and logistic support to ISIL…”, Sehemu ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Bi.Clinton.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa huenda kilichoandikwa kwenye ujumbe huo kina ukweli ndani yake kwani nchi kama Saudia Arabia pekee imefadhili kampeni za Bi.Clinton kwa %20,huku Qatar ikiwa miongoni mwa nchi zinazomuunga mkono Bi.Clinton.
Hata hivyo Wafuasi wa Bi.Clinton wanaamini taarifa hiyo ya Mtandao huo,uliofungiwa nchini humo ni mpango wa kumchafulia jina Bi.Clinton.
Uchaguzi Mkuu wa Rais Marekani utarajiwa kufanyika Novemba 8 mwaka huu,huku kipute kikiwa baina ya Bi.Clinton anaekiwakilisha Chama Cha Democtratic anachotoka Rais Obama,na Mfanyabiashara Donald Trump anaewania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Republican.