Thursday, November 3, 2016

TANZIA (VIDEO):Mwanafunzi abakwa hadi kufa,Wenzake wamwelezea,wadai alikua na kipaji cha muziki.

ARUSHA- Mapema tarehe 2,Mwezi November 2016 zilisambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).



Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho  amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya Leo akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo hicho.


Kiongozo huyo wa Serikali ya Wanafunzi Chuoni hapo akihojiwa na @DjHazoo wa Radio 5,amedai kuwa Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo hasa ikizingatiwa kuwa Marehemu alikua na kipaji kikubwa cha kuimba.

Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.

Hata  hivyo inasubiriwa ripoti ya uchunguzi kutoka kwa jeshi la Polisi juu ya tukio hilo lililolaaniwa vikali na Wananchi kote nchini.

.....!! WHERE IS THE LOVE ..?

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.