Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe katika kipindi cha
Maswali kwa Waziri Mkuu leo amedai kuwa, mnamo siku ya Jumanne tarehe
25/10/2016 saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM ambacho
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mwenyekiti, na kilihudhuriwa na
Katibu MKuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa ajili ya kujadili Muswada wa
Habari.
Mbowe amesema kuwa Wabunge wakiwemo Mawaziri walihongwa shilingi milioni
10 kila mmoja ili waweze kusaidia kupitisha Muswada wa Habari
unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni ili kujadiliwa.
Hata hivyo,Naibu spika alikataa katakata Waziri mkuu kujibu swali la Mbowe
kwa waziri mkuu kuhusu tuhuma hizo za wabunge wa CCM kuitwa kwenye kikao
na kupewa fedha kiasi cha milioni 10 kila mmoja ili wasiibane serikali
kwenye muswada wa sheria unaotarajiwa kuwasilishwa tarehe 4 Mwezi Novemba,2016.
Maelezo ya Naibu spika ni kuwa swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa tuhuma hizo ni za rushwa kwa wabunge.