Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini, Neema Tarimo amefikishwa mahakamani
jijini Arusha na kusomewa shtaka la kumtukana Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo
baada ya kumtumia ujumbe kwenye simu yake wenye neno 'shoga'.
Mke wa Mbunge huyo amekana kumtusi Mkuu huyo wa Mkoa baada ya kudai kuwa neno shoga sio tusi bali ni neno ambalo hulitumia kuwaita marafiki zake na kuongeza kuwa neno shoga kwenye mazingira ya Tanzania humaanisha rafiki.