Showing posts with label Ligi Kuu Uingereza. Show all posts
Showing posts with label Ligi Kuu Uingereza. Show all posts

Saturday, September 10, 2016

Video:Arsenal na Man City mwendo mdundo,Morinho hoi kwa Guardiola.

 
Bao la dakika ya 90 la mkwaju wa penati kupitia kwa Santi Cazorla limeinusuru Arsenal kupata sare katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates dhidi ya Southampton baada ya kushinda mabao 2-1.
Southampton walianza kupata goli katika dakika ya 18 baada ya kipa wa Arsenal Petr Cech kujifunga mwenyewe kufuatia mpira uliotokana na adhabu ndogo uliopigwa na Dusan Tadic kugonga mwamba na kumgonga mgongoni.

Laurent Koscielny aliisawazishia Arsenal bao safi dakika ya 29 baada ya kupiga overhead kick nzuri baada ya mpira uliotokana na kona kuzagaazagaa langoni mwa Southampton.
Santi Cazorla ndiye shujaa wa Arsenal ambaye alifunga bao la pili kwa penati baada ya Olivier Giroud aliyeingia kutoka benchi kuchezewa madhambi na beki wa Southampton Jose Fonte.



Katika mchezo mwingine,Jose Mourinho ameendeleza rekodi mbaya mbele ya Pep Guardiola baada ya kushuhudia timu yake ya Manchester United ikiwa nyumbani ikifungwa 2-1 dhidi ya Manchester City.
Dalili za United kupoteza zilianza mapema kufuatia Man City kuanza mpira na kasi kubwa huku wakipiga pasi nyingi na za uhakika zilizowapoteza kabisa Man United hasa kwenye eneo la kiungo.
Man City walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Kevin de Bruyne dakika ya 15 baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Kelechi Iheanacho.


 City waliongeza tena bao la pili kupitia kwa Kelechi Iheanacho dakika ya 36 baada ya kuuganisha mpira uliogonga mwamba baada ya kazi nzuri ya Kevin de Bruyne.
Man United walipata goli la pekee kupitia kwa Zlatan ambaye aliunganisha mpira uiotemwa kimakosa na kipa wa City Claudio Bravo.



 Mambo manne kuhusu vilabu hivi mahasimu wa Jiji la Manchester.
  • Jose Mourinho ameshinda mechi tatu kati ya 17 alizokutana na Pep Guardiola (sare 6 Lkafungwa 8).
  • Manchester City wamepata ushindi wao wa 50 kwenye deeby ya Manchester katika jumla ya michuano yote.
  • Dhidi ya Man City, Man Utd hii ni mara ya nne kumiliki mpira kwa kiasi kidogo wakiwa uwanja wao wa nyumbani tangu msimu wa 2003-04 (39.9%).
  • Kevin de Bruyne amehusika moja kwa moja kwenye magoli 32 katika mechi 46 kwenye michuano yote kwa Man City (magoli 17, pasi za magoli 15).
  • Kelechi Iheanacho amefunga magoli nane kutokana na mashuti 13 yaliyolenga lango kwenye Premier League.
 Matokeo ya michezo mingine.



Thursday, September 8, 2016

VIDEO:Zlatan Ibrahimovic amtumia zawadi mlinda mlango wa Man-City.

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ameendeleza majivuno yake na kujitabainisha kama mtu mwenye dhihaka sana baada  kupost  video kwenye ukurasa wake wa  Instagram akimpa onyo golkipa mpya wa Manchester City Claudio Bravo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaowakutanisha watani hao wa jiji la Mancherster  wikend hii.
 Katika video hiyo  Zlatan Ibrahimovic ambayo anaonekana akiandika ujumbe kwenye boksi lenye vifaa maalum alivyomuandalia mlinda mlango mpya wa klabu ya Manchester City Claudio Bravo.

Juu ya boksi hilo ameandika hivi;
Welcome to Manchester! Here’s some training gear, you’re gonna need it. See you Saturday.#MUFC #ManchesterDerby


Wednesday, September 7, 2016

Eden Hazard mchezaji bora wa mwezi ligi kuu Uingereza.

Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard ameshinda Tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi wa August katika ligi kuu nchini Uingereza akiwashinda Antonio Valencia wa klabu ya Manccherster United,,Raheem Sterling kutoka Mancherster City na Curtis Davies wa Hull City.
   Hazard ambaye amefunga magoli 2 katika mwezi huo kunako ligi hiyo, amepata asilimia 41 ya kura zilizopigwa, Valencia asilimia 34, Sterling akipata asilimia 17 huku Curtis Davies akipata asilimia 8.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.