Bao la dakika ya 90 la mkwaju wa penati kupitia kwa Santi Cazorla limeinusuru Arsenal kupata sare katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates dhidi ya Southampton baada ya kushinda mabao 2-1.
Southampton walianza kupata goli katika dakika ya 18 baada ya kipa wa Arsenal Petr Cech kujifunga mwenyewe kufuatia mpira uliotokana na adhabu ndogo uliopigwa na Dusan Tadic kugonga mwamba na kumgonga mgongoni.
Laurent Koscielny aliisawazishia Arsenal bao safi dakika ya 29 baada ya kupiga overhead kick nzuri baada ya mpira uliotokana na kona kuzagaazagaa langoni mwa Southampton.
Santi Cazorla ndiye shujaa wa Arsenal ambaye alifunga bao la pili kwa penati baada ya Olivier Giroud aliyeingia kutoka benchi kuchezewa madhambi na beki wa Southampton Jose Fonte.
Dalili za United kupoteza zilianza mapema kufuatia Man City kuanza mpira na kasi kubwa huku wakipiga pasi nyingi na za uhakika zilizowapoteza kabisa Man United hasa kwenye eneo la kiungo.
Man City walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Kevin de Bruyne dakika ya 15 baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Kelechi Iheanacho.
City waliongeza tena bao la pili kupitia kwa Kelechi Iheanacho dakika ya 36 baada ya kuuganisha mpira uliogonga mwamba baada ya kazi nzuri ya Kevin de Bruyne.
Man United walipata goli la pekee kupitia kwa Zlatan ambaye aliunganisha mpira uiotemwa kimakosa na kipa wa City Claudio Bravo.
Mambo manne kuhusu vilabu hivi mahasimu wa Jiji la Manchester.
- Jose Mourinho ameshinda mechi tatu kati ya 17 alizokutana na Pep Guardiola (sare 6 Lkafungwa 8).
- Manchester City wamepata ushindi wao wa 50 kwenye deeby ya Manchester katika jumla ya michuano yote.
- Dhidi ya Man City, Man Utd hii ni mara ya nne kumiliki mpira kwa kiasi kidogo wakiwa uwanja wao wa nyumbani tangu msimu wa 2003-04 (39.9%).
- Kevin de Bruyne amehusika moja kwa moja kwenye magoli 32 katika mechi 46 kwenye michuano yote kwa Man City (magoli 17, pasi za magoli 15).
- Kelechi Iheanacho amefunga magoli nane kutokana na mashuti 13 yaliyolenga lango kwenye Premier League.