Kampuni ya Acer ya nchini Taiwan, imeweke rekodi baada ya kuzindua
Laptop ya kwanza (Predator 21X) yenye kioo chenye mikunjo.
Kampuni hiyo imesema kuwa, Laptop hiyo yenye kioo cha ukubwa wa inchi
21 kitasaidia kwenye baadhi ya michezo ya video kwa kutumia kioo hicho.
Hata hivyo Laptop hizi zitaanza kupatikana Januari mwakani ambapo kwa mujibu wa kampuni hiyo, wateja wa awali watatakiwa kutoa oda kwanza ndipo zitengenezwe.
Licha ya muonekano wa laptop hizi kuwashangaza watu wengi,maafisa wa kampuni ya Acer wamefurahishwa na ugunduzi na kuongeza kuwa hata kama bidhaa yao haitafanya vizuri sokoni
lakini wao watajivuni ufumbuzi wa teknolojiwa walioufanya.