Rodrigo “Digong” Duterte ni kiongozi ambaye msimamo wake na matamshi
yake huzua utata mara kwa mara. Amegonga vichwa vya habari tena baada ya
kuonekana kumtusi Rais wa Marekani Barack Obama na kumuita “mwana wa
kahaba”.
Duterte aliweza kukabiliana na utata juu yake na kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Ufilipino wa mwezi Mei.
Baada ya kula kiapo cha urais, Juni 30 Bw Duterte, ambaye kipindi
kirefu aliishi mjini Davao kusini mwa nchi tangu aliposhinda, ana
mamlaka ya kuongoza taifa hilo kwa muhula mmoja wa miaka sita.
Rodrigo “Digong” Duterte alizaliwa mnamo mwaka 1945 katika familia iliyojikita katika siasa za ndani ya nchi ambapo kwa wakati mmoja baba yake alikuwa gavana wa jimbo na huku familia yao ikitajwa kuwa na uhusiano na familia zenye ushawishi mkubwa za Duranos na
Almendrases katika jimbo Cebu, ambako baba yake aliwahi kuwa meya.
Bw Duterte amesomea taaluma ya sheria na alipanda cheo hadi kuwa
mwendesha mashtaka kabla ya kuteuliwa kuwa naibu meya wa Davao wakati wa
mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Ferdinand Marcos mwaka 1986.
Wafuasi wa Duterte wanasema sifa yake ya ukali ndio wafilipino wanayohitaji ili kukabiliana na ufisadi na uhalifu.
Alijijengea umaarufu kwa kupiga vita baadhi ya matatizo makubwa
yanayowakabili Wafilipino – uhalifu, makundi ya uasi, na ufisadi. Yote
haya yalipungua kwa kiwango kikubwa wakati alipokuwa kiongozi wa Davao,
na kufanya mji huo kuwa mmoja wa miji salama zaidi nchini Ufilipino.
Alikuwa meya mwaka 1988 na kushikilia wadhfa huo kwa kipindi cha
miaka 10, kabla ya kushinda kiti cha ubunge katika Bunge la Congress kisha akarejea kwenye kiti cha umeya mwaka 2001.Duterte ambaye utawala wake ni wa kipekee,anaelezewa kama kiongozi mwenye
sera za Kijamaa na mwanamageuzi ambae sera zake za uchumi zilikuwa
si za kuaminika wakati wa kapeni zake.
Utawala wake na misimamo yake.
Aliahidi kubadili mfumo wa utawala wa taifa kutoka kwa mfumo wa bunge
moja kuu yenye hadi kwenye mabunge ya majimbo, ili kugawana vyema mali
ya taifa.
Msemaji wake alisema kutakuwa na “mageuzi makubwa yatakayofanyiwa katiba ya nchi”.
Pia alikuwa ameahidi “kuwaua wahalifu 100,000” akiingia ikulu na kudai kuwa atatoa ruhusa kwa vikosi vya usalama mamlaka ya “kupiga
risasi na kuuwa” washukiwa wa uhalifi wanaokwepa kukamatwa hasa wale wa madawa ya kulevya.
Tayari kufikia sasa, washukiwa 2,5000 wameuawa.
Tabia yake ya kuwatusi watu.
Amewahi kutangaza hadharani kwamba Ufilipino, ambayo imekuwa mshirika mkuu wa Marekani, haitategemea sana Washington.
Kijamii, yeye huunga mkono wapenzi wa jinsia moja lakini ni
mhafidhina katika masuala mengi ya kijamii. Amegusia kupiga marufuku
unywaji pombe maeneo ya wazi na kutoa amri ya kutotoka nje kwa vijana.
Amekuwa akiwatusi watu mashuhuri. Alimwita Papa Francis “mwana wa
kahaba” huku akijua wazi kuwa Ufilipino ni taifa lenye Wakatoliki wengi.Amewahi kumtusi pia
waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa kumuita
“mwendawazimu” na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino
kama “mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba”.
Alifanya mzaha na kusema kwamba alipokuwa meya angekuwa mtu wa kwanza
kumbaka mmishenari kutoka Australia aliyeuawa wakati wa fujo gerezani.
Kuwaua wanawe.
Alisema kwenye mdahalo wa televisheni kwamba anaweza kuwauwa wanawe kama watatumia mihadarati.
Yote hayo yamemuongezea sifa miongoni mwa wananchi wengi nchini Ufilipino kama
mtu anayeweza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mambo muhimu
yanatekelezwa .
Amekuwa akilinganishwa na mgombea wa urasi wa Marekani Donald Trump,
lakini alikataa kufananishwa naye,akisema kwamba Trump ni mtu asieshaurika.
Bw Duterte ameoa mara mbili, ana watoto wanne, na miongoni mwao binti
yake Sara – alikuwa meya kwa muhula mmoja kabla ya kurejea tena kwa
baba yake .
Kwa sasa hana mke, lakini anadai kuwa na marafiki kadhaa wa kike.
Chanzo:bbcswahili.