Tuesday, September 13, 2016

Picha:Uzinduzi wa filamu ya "Queen Of Katwe",Lupita Nyongo na hisia za wanawake wa kiafrika.

                                                                    
Wikend iliyopita Sept.11,Mwigizaji raia wa Kenya na mshindi wa tuzo ya Oscer Lupita Nyongo mbele ya mamia ya ya watazamaji alitambulisha filamu yake mpya inayofahamika kama Queen Of Katwe katika tamasha kubwa la filamu nchini Marekani linalofahamika kama Toronto International Film Festval  ambapo katika filamu hiyo ameshirikiana na mwigizaji nguli David Oyelowo,kwa wale wapenzi wa filamu watamkumbuka alivyocheza nafasi ya Martin Luther King Jr katika filamu ya SELMA ila pia katika filamu hii yupo muigizaji chipukizi,binti wa miaka 11 Madina Nalwanga.

  “It’s a challenge, especially not being (a mother) myself and that’s one of the reasons why I wanted to do it,” .......... “I thought it was such a stretch for me, and I like stretching myself and challenging myself, and trying things I haven’t done before.”Lupita Nyongo alizungumza hayo kwenye mahojiano na repoter wa mtandao wa People.com

                                     Lupita Nyongo na David Ayelowo.

 
 Kwa kifupi filamu hii  imebeba simulizi ya binti alizaliwa kwenye familia yenye maisha duni ambapo akiwa na miaka 11 alikumbana na changamaoto nyingi na kufanikiwa kupata elimu  katika mazingira magumu na hatimae binti huyu  anakua shujaa na kuwa sehemu ya mabadiliko kwenye jamii yake.Hii sio filamu ya kukosa kuitazama kwani imefanyika kwenye ardhi ya Uganda.

Filamu hii itapatikana sokoni na kuanza kuoneshwa kwenye majumba ya filamu "Theatre" kuanzia Sept.23


Tazama baadhi ya picha kwenye uzinduzi huo; 


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.