Showing posts with label Dar es salaam. Show all posts
Showing posts with label Dar es salaam. Show all posts

Wednesday, November 16, 2016

PICHA:Barabara ya bilioni 4 za sherehe za Uhuru kama inavyoonekana kutoka angani.


Wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru Disemba 9 mwaka huu,Rais Magufuli alifuta sherehe za uhuru na kuagiza kiasi cha fedha takriban bilioni 4 zilizopangwa kuratibu sherehe hizo kutumika kwenye mradi wa upanuzi wa barabara eneo la kutoka  Morocco hadi Mwenge jijini Dar es salaam,huku akiwataka wananchi kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa taifa letu kwa kufanya usafi kwenye maeneo yao.


Huu ni muonekano wa juu wa barabara hiyo iliyopanuliwa na kuruhusu magari mawili kwenda na kurudi kwa wakati mmoja.


VIDEO:Padri akamatwa na gari ya wizi.


Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salam, Simon Siro akizungumza na waandishi wa habari  amesema wamewakamata wezi wanne wa magari akiwemo Padri wa kanisa katoliki Parokia ya Sumbawanga ambae anahojiwa na jeshi hilo.

Aidha ameongeza kuwa wamekamata vizuizi vyenye misumari vilivyokua vikiwekwa barabarani ili kusababisha magari kupata ajali na kuyapora maeneo ya Mbweni jijini hapa na kutoa  onyo kwa watu wanaofanya mchezo huo.

Tuesday, November 1, 2016

Boniface Jacob (CHADEMA) ashinda nafasi ya Umeya Ubungo.



Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob ameshinda nafasi ya Umeya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo baada ya ule wa awali kuhairishwa.

Amepata ushindi wa jumla ya kura  16 za UKAWA na kura 2 CCM huku Naibu Meya akishinda kwa kura 15 dhidi ya kura 3.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya kuundwa kwa Manispaa mpya ya Ubongo iliyokua ndani ya Manispaa ya Kinondoni ambayo Jacob awali alikua Meya wa Manispaa hiyo.

Wachina walizwa Sh22.8 milioni na tapeli aliejitambulisha kama Paul Makonda.

Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye  ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda.

Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia huyo atoe Dola 3,500 za Marekani kwa ajili ya msaada wa kumsomesha mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manilla kilichopo nchini Ufilipino.

 “Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jensen Hung (39) alikubali ombi la mkuu wa mkoa huyo feki na kumtuma msaidizi wake, Marco Li aende ofisini kwake kwa ajili ya kujiridhisha,” alisema Kamanda  Sirro.

Sunday, October 23, 2016

UKAWA wasusia uchaguzi wa Meya Kinondoni,Wagombea wa CCM wapita bila kupigwa.




Madiwani wa vyama vinavyounda umoja wa  UKAWA wamesusia uchaguzi wa Meya na naibu meya wa Halmashauri ya manisapa ya Knondoni,uliofanyika Oktoba 23,2016 hali iliyopelekea wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

Wabunge hao wa upinzani wamesusia uchaguzi huo wakinukuu sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 ambazo  haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja.

Wabunge waliolalamikiwa ni pamoja na Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga ambao waliapishwa kama madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

CCM wamemchagua Benjamini Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho ambapo George Manyanya amchagiliwa kuwa Naibu Meya.

Wednesday, October 12, 2016

Aliekua Meya wa Jiji la Dar es salaam afariki dunia,Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi.

Aliekua Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Dkt.Didas Masaburi amefariki dunia usiku wa Oktoba 12.



Dkt.Masaburi alikua amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini haikuelezwa alikua akisumbuliwa na maradhi gani.

Dkt.Masaburi alikua Meya wa Jiji la Dar es salaam kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 ambapo aliacha wadhifa huo na kujitosa kwenye mbio za kuwania ubunge wa jimbo la Ubungo katika uchanguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM),lakini alindwa baada ya mpinzani wake kwa tiketi ya CHADEMA,Said Kubenea kuibuka mshindi.

Mbali na kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam,Dkt.Masaburi amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kumuelezea Dkt.Masaburi kama masomi mzuri na kiongozi alielitumikia taifa na kusimamia anachokiamini.

Thursday, October 6, 2016

"Scopion",anaedaiwa kumtoboa mtu macho afanya vituko mahakamani.

Salum Henjewele (34) maarufu kama "Scorpion" mkazi wa Yombo Machimbo anaetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho Said Mrisho jana aliwashangaza watu mara baada ya kufanya vituko mahakamani alipokua akisomewa mashtaka yanayomkabili.

Scopion ambae ni mwalimu wa mchezo wa mashwati (karate) alimfanyia unyama huo Said mnamo Septemba 6 mwaka huu eneo la Buguruni Sheli Jijini Dar es Salaam.


Katika hali ya kushangaza,mtuhumiwa huyo alibadilisha mavazi yake akiwa Mahakamani ili asijulikane mbele ya umati wa watu waliokua wamefurika Mahakamnii hapo.Akiwa anatoka mahakamani Scopion alionekana amevaa mavazi tofauti  na yale aliyokua amevaa asubuhi wakati kesi yake ilipokua ikitajwa.

Awali Scopion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore  kwa kuongozwa na wakili wa serikali  Munde Kalombola na kumsomea mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kumsababishia upofu wa kudumu Said Mrisho kwa kumtoboa macho.

Hata hivyo shauri hilo limeahiriishwa hadi Oktoba 19 mwaka huu litakapotajwa tena ambapo kwa mujibu wa hati hiyo ya mashtaka ya kesi hiyo namba 276 ya mwaka 2016 ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 28 mwaka huu ambapo hata hivyo wakati akisomewa mashtaka yake yake,mtuhumiwa huyo alionekana mtu asiye na wasiwasi huku akitabasamu muda wote.

Inadaiwa kuwa mnamo Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli,Manispaa ya Ilala,Dar es salaam,mtuhumiwa aliiba cheni ya silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh.60,000 na "black bend" ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh.330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh.474,000 mali ya Said Mrisho aliemtia upofu kwa kumtoboa macho,ambapo wakali wa serikali aliongeza kuwa kabla kutekeleza tukio hilo mtuhumiwa alimjeruhi Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo machoni,tumboni na mabegani ili kurahisishwa kupora mali hizo.

Mama mzazi wa Mrisho;

Nje ya mahakama hiyo,mashuhuda wa Shirika la Wambea Duniani,(Shilawadu) walimuona mama mzazi wa mrisho aitwaye Halima Jissu pamoja na ndugu na jamaa zake wakilia muda wote huku wakisema wanamwachia Mungu kwa kilichotokea.




Wednesday, September 7, 2016

Alietishia kuipindua Ikulu afikishwa Mahakani.

SERIKALI imemfikisha mahakamani mfanyabiashara Leonard Kamili maarufu kama"Materu" (31) kwa tuhuma za kutishia kuipindua Ikulu kwa maneno,mshtakiwa huyo anayedaiwa kutoa maneno hayo kwa nia ya kumtisha Rais Dk. John Magufuli alifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Margareth Bankika ambapo mshatakiwa huyo mkazi wa Moshi Baa kwa Diwani, jijini Dar es Salaam, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo aliedai  mshtakiwa huyo alichapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.


Akisoma mashtaka hayo Lukondo alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, Julai 17, mwaka huu sehemu isiyofahamika jijini Dar es Salaam ambapo mshtakiwa huyo  huku akijua kuwa ni kosa alichapisha taarifa  na kuiweka katika mtandao huo ikiwa na maneno ya uongo yasemayo: “Magu ajiandae tunaenda kupindua mpaka Ikulu” alisema.
 Inadaiwa ujumbe huo ulikuwa na nia ya kumtishia Rais Dk. John Magufuli.
Mshtakiwa akiwakilishwa na Wakili Neema Lamwai, alikana kutenda kosa hilo, ambapo Wakili wa Serikali Diana alidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa kutajwa.
Hakimu Margareth alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambayo yalimtaka awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja na mshtakiwa huyo kutimiza masharti ya dhamana, hivyo ameachiwa kwa dhamana hadi Septemba 20, mwaka huu, kesi itakapotajwa tena.

Na Kulwa Mzee-Mtanzania.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.