Showing posts with label Bongofleva. Show all posts
Showing posts with label Bongofleva. Show all posts

Thursday, November 3, 2016

U - HEARD | Usipotamani Msambwanda Wa Masogange Utakua Mchele - Dogo Janja

Habari zilizopo mezani kwa mhariri mkuu wa makorokocho Soudy Brown ni report za kuwepo kwa fununu za kuwepo kwa penzi jipya kati ya rapper  Dogo Janja mwenye Kidebe chake na malkia wa vichupa vya bongoflava Agnes Masogange.

janjaro

Fununu hizo zilizagaa haraka kwa speeda ya umeme mara baada ya Dogo Janja (Janjaro) kama anavyojiita siku hizi kupost picha ikimuonyesha Masogange akilingishia Msambwanda kwenye FaceTime ambayo moja kwa moja ilitafsriwa kama wawili hao walikua kwenye convo ya hatari.

Baada ya kumtafuta Janjaro afungukie ishu hiyo, Dogo alikua na haya ya Kujitetea:

Thursday, September 8, 2016

Diamond,Ali Kiba na Ya Moto Band watajwa kuwania tuzo za Afrima.

Tuzo za Afrima zinazoandaliwa kwa ufadhili wa taasisi ya African Union Commission (AUC)     zimetangazwa huku orodha kamili ya wasanii wanaowania tuzo ikimjumuisha Msanii wa Bongo Fleva,
Diamond anaewania vipengele vitano.

Viepengele hivyo ni pamoja na  Songwriter of The Year in Africa, Song of The Year in Africa, Artiste of The Year, Best Artist in Africa na Best Male Artist in Eastern Africa.

Watanzania wengine waliotajwa kwenye tuzo hizo ni pamoja na Alikiba anayewania cha Best Male Artist in Eastern Africa na Yamoto Band likitajwa kuwania kipengele cha Revelation of The Year.
Tazama orodha kamili,


 afrima



afrima1

afrima2

afrima4
afrima5afrima4afrima6afrima3


afrima8
 afrima9

"Sina haraka ya kuzaa na Jux" - Vanessa Mdee.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Televison Vanessa Mdee amedai kuwa hana haraka ya kupata mtoto na mpenzi wake Jux na kudai kwa sasa wapo watoto wengi wa kulea akiwepo mtoto wa Diamond Platnumz, mtoto wa Shetta pamoja na mtoto wa mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Dullah,na kuongeza kuwa wote hao ni kama watoto wake.


 “Kiukweli sina haraka ya kupata mtoto na Jux kwani saizi bado kuna watoto wengi wa kuwalea kama mtoto wa Diamond, Shettah na mtoto wako Dullah kwani wote hao kwangu ni kama wanangu tu”.Alisema Vanessa

Mbali na hilo Vanessa Mdee alisema kuwa mara nyingi anajitahidi kufanya media tour katika nchi za watu kutokana na ukweli kwamba watu wa nje ni wazito sana kupokea kazi za wasanii ambao siyo wao.

“Unajua nafanya sana media ‘tour’ kwani wenzetu ni wazito sana kupokea kazi za wasanii wa nje ya kwao, hivyo hizo media tour zinanisaidia kujenga Fan Base katika nchi zao, kuongeza mzunguko wa kazi zangu kuchezwa kwao, hata kutafuta mashavu mengine” alisema Vanessa Mdee.

V-money kuungana na mastaa wa muziki Afrika kwenye tamasha kubwa nchini Marekani.

Hiyo itakuwa show ya pili inayowakutanisha mastaa wa muziki kutoka barani Afrika baada ya ile ya awali iliyofanyika July 22, kwenye ukumbi wa Barclays Centre, New York, Marekani na kukutanisha mastaa kama Diamond, Wizkid, Davido, Tiwa Savage, Flavour na wengine.

Katika show ya October 22, Vanessa Mdee atakua sehemu ya wasanii wakubwa wa Afrika watakao panda jukwaani wakiwemo 2 Face, Flavour, P –Square, D’Banj, Kcee, Mafikizolo, Fally Ipupa na Cabo Snoop.

"Houston we have a PROBLEM!!!!! See you at the Toyota Centre on the 22nd Oct 2016." Ameandika Vee Money kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

                                                   Vanessa Mdee & 2 Face.

Wednesday, September 7, 2016

AUDIO:"Hata P-Funk alinyoosha mikono kwa Daz Naledge"-Jay Mo.


                                                     
Mmoja wa ma-rapper wakongwe nchini Jay Mo amemuelezea producer Daz Naledge alietengeneza hit song ya "Pesa Madafu" kama miongoni mwa watayarishaji wenye uwezo na kipaji kikubwa.

                                                            Daz Naldge.

Jay Mo amedai kuwa sio jambo rahisi kwa mtu kama P-Funk,anaetajwa kama mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini kukubali mtayarishaji mwingine kuitumia studio yake  na kuongeza kuwa P-Funk ndie alieridhia mdundo huo wenye mahadhi ya "Trap" usukwe upya kwenye studio za Bongo  Records mara baada ya kuusikia mdundo wa awali uliotengenezwa na Naldge ambae wakati huo alikua akiendesha shughuli zake za muziki jijini Arusha
                                                        Jay Mo.

Msikilize Jay Mo  hapahttp://www.audiomack.com/song/mdadisitzrapper/jay-more-akielezea-jinsi-p-funk-alivyompokea-producer-daz-naledge

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.